Munya amesema Ruto amekuwa kikwazo kwa ajenda ya serikali kwani amekuwa akiwachochea maseneta na wabunge kusababisha vurugu serikalini na kufanya kuwa vigumu wa rais Uhuru Kenyatta kutekeleza majukumu yake ya utawala . Mirengo miwili ya kisiasa imeibuka ndani ya chama tawala cha Jubilee kati ya wanaomuunga mkono rais Kenyatta na walio katika upande wa naibu wake William Ruto na kuunda makundi ya Tangatanga na Kieleweke.
Akizungumza katika mkutano na wakulima wa kahawa huko Meru siku ya jumamosi Munya amesema rais Kenyatta hajakiuka sheria au katiba kwani anatumia maamlaka yake kufanikisha demokrasia .Munya amesema kuondolewa kwa Kindiki Kithure kama naibu spika wa senate ni jambo linalokubalika kwani seneta huyo alikuwa amemkaidi kiongozi wa chama chake .siku ya ijumaa maseneta 54 kati ya 67 walipiga kura kumuondoa Kindiki kutoka wadhifa huo .
Wale waliopiga kura kumuokoa Kindiki ni Kipchumba Murkomen wa Elgeyo Marakwet, Susan Kihika wa Nakuru, Samson Cherargei wa Nandi, Aaron Cheruiyot wa Kericho, Christopher Lang'at wa Bomet na Mithika Linturi wa Meru.Kindiki wakati mmoja alikuwa ametajwa kama anayeweza kuwa mgombea mwenza wa naibu wa rais William Ruto wakati wa uchaguzi mkuu wa 2022 na kuondolewa kwake kama naibu spika wa senate ni pigo kwa mrengo wa DP
Munya amesema hatua ya kuondolewa kwa Murkomen na susan Kihika katika uongozi wa senate ni dhihirisho kwamba rais Kenyatta analenga kukinadhifisha chama cha Jubilee ili kuboresha ajenda yake ya maendeleo na usimamizi ufaao wa shughuli za serikali .
Nafasi zao zilichukuliwa na Samuel Poghisio wa West Pokot na seneta wa Murang’a Irungu Kang’ata,
Munya amesema kila mtu anafaa kuubeba msalaba wake na kufuata mkondo anaotaka kinara wa chama cha Jubilee na Mkuu wa serikali ,Uhuru Kenyatta