Not Guility:Trump apatikana bila hatia na bunge la senate la Marekani

Rais Wa Marekani Donald Trump
Rais Wa Marekani Donald Trump
Rais Donald Trump wa Amerika ameondolewa makosa yote  katika mchakato wa kumwondoa madarakani kupitia kura ya senate  katika  kufikisha tamatai utaratibu wa kumuonyesha mlango kabla ya kumalizika kwa kipindi chake afisii .Senate,  inayoongozwa na wanachama wengi wa chama cha Trump  cha run Republican,  ilipiga kura  kumpata bila hatia rais huyo kwa kura 52 dhidi ya 48  kuhusu kutumia vibaya maamlaka yake kura 53 kwa 47 kuhusu madai ya kuzuia Congress kufanya kazi yake .

Wanachama wa Democrats  walimshtaki rais Trump  disemba kwa madai ya kuishinikiza Ukraine kumchunguza  anayeweza kuwa mpinzani wake katika uchaguzi ujao wa urais  ili kumchafulia jina kabla ya kura.

Katika kura hiyo ya kihistoria Senate iliamua kutomuodnoa afisini Bwana  Trump ambaye anagelazimika kumkabidhi maamlaka makamu wake Mike Pence endapo mashtaka dhidi yake yangeidhinishwa . Trump anayetafuta muhula wa mwisho na wa pili Novemba tarehe 3 amekuwa akikanusha kufanya kosa lolote . Amekuwa akidai kwamba wanachama wa democrat wana hila dhidi yake na hiyo basi kuwa na uchu wa kutafuta kila fursa ya kumuondoa afisini .