Trump amejibu madai hayo kupitia Twitter kwa kusema kwamba hajawahi kukutana na E Jean Carroll, na kwamba tukio hilo ‘halikuwahi kufanyika’. Kulingana na Carrol ,dhulma hiyo ilifanyika kati ya mwaka wa 1995 au 1996 wakati Trump alipokuwa mdau kumbwa katika sekta ya ujenzi wa majumba naye mwandihsi akiliandikia jarida moja kando na kuwa mtangazaji wa kipindi cha televisheni .
Ufichuzi huo uliotolewa katika kitabu cha Carrol kilichochapishwa ijumaa kinamfanya kuwa mwanamke wa 16 kudai kudhulumiwa kimapenzi na rais huyo wa Marekani .Carroll ambaye sasa ana umri wa miaka 75, amesema alikutana na Trump katika duka la nguo la Bergdorf Goodman huko Manhattan walipokuwa wote wakinunua nguo . Amesema mwanzoni mazungumzo yao yalikuwa ya kirafiki wakati Trump alipotaka ushauri wake kuhusu vazi la ndani alilotaka kumnunulia mwanamke ambaye hakumtaja . Kisha kwa utani walipendekeza kwamba kila mmoja wao angelijaribu kuvalia vazi hilo.
" Pindi mlango wa chumba cha kubadilisha kilipofunguka , alinijia kwa nguvu na kunisukuma ukutani,nikapiga kichwa changu kwa uchungu kwenye ukuta kisha akaiweka mido yake kwenye yangu ’ Carrol ameandika . Baada ya kumbana ukutani Carrol anasema Trump aliendelea kumfunua vazi lake ,akajifungua long’i kisha akamwingilia kutumia uume wake-wakati wote Trump alikuwa bado amevalia nguo zake hadi Carrol alipomudu kumsukuma na kisha kukimbia kutoka chumba hicho cha kubadilisha .Carroll hakuripoti kisa hicho kwa polisi kwa sababu anasema alihofia matokeo yake .
Ameandika kwamba aliogopa kujitokeza hadharani kusema kilichotokea kwa ajili ya kuogopa ‘kupokea vitisho vya kuuawa ,kutoroshwa kutoka kwake,kupuuzwa au kupakwa tope’