nuno.espirito

Nuno Espirito Santo apigiwa upato kuwa meneja wa Arsenal

Meneja wa Wolves Nuno Espirito Santo ndiye meneja aliye mstari wa mbele kuchukua nafasi ya Unai Emery kama meneja wa Arsenal (Mail)

Wahudumu wa Arsenal wanaamini kuwa kocha Unai Emery atafutwa kazi , lakini bado anatarajiwa kuongoza timu katika mechi ya Ligi ya Uropa dhidi ya Eintracht Frankfurt. (Goal)

Ikiwa watashindwa kuichapa Frankfurt, na Norwich City siku ya Jumapili , Emery atapoteza kazi (Express)

Mourinho: Mashabiki wa Arsenal, Chelsea na United watoa hisia zao

Manchester City imeanzisha mazungumzo na mshambulizi Raheem Sterling kuhusu kandarasi mpya. Sterling alitia sahihi mkataba mwezi Novemba mwaka 2018 ambao unafaa kukamilika mwaka 2023, haja ya City ikiwa ni mustakabali wake.

Endapo kandarasi hiyo itatekelezwa, Raheem atakuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa kitita kikubwa cha fedha kwenye ligi kuu ya uingereza.

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp hana wasiwasi wowote kuhusu hali ya Mohamed Salah ila itabidi Liverpool kuwa na subira kabla ya kuamua iwapo mshambulizi huyo atacheza dhidi ya Napoli.

Salah hakuruhusiwa uwanjani licha ya kuwa mchezaji wa akiba wakati Liverpool iliilima Crystal Palace mabao mawili kwa moja Jumamosi iliyopita, baada ya Klopp kudokeza kuwa jeraha la goti la mshambulizi huyo lilikuwa halijapona.

West Ham wanaangalia uwezekano wa kumchukua meneja wa Sheffield United Chris Wilder kama meneja wao, ikiwa wataamua kumfuta kazi meneja wao sasa Manuel Pellegrini.

Rekodi ya asilimia 100 ya Arsenal yafika kikomo katika ligi ya Europa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments