Nviiri aeleza ujio wake katika sanaa. Awazungumzia SautiSol

IMG_0081__1568293429_77995
IMG_0081__1568293429_77995
Staa wa muziki kutoka nchi jirani ya Uganda Nviiri amefunguka jinsi alivyojipata akifanya kazi na kundi la Sauti Sol.

Nviiri alipatana na mastaa hawa wa hapa nchini katika studio na pale wakaanza mazungumzo.

Soma hadithi nyingine hapa:

"Tulikuwa tunawork kwa studio...Nikafanya projects kadhaa wakatambua uwezo wangu wa kuandika nyimbo. Kutoka hapo tukaanza kuandika pamoja Melanin."

Nviiri yupo kwenye lebo ya Sol generation.

Lebo hii inamilikiwa na kikundi cha Sauti Sol na kimeweza kuwasaini mastaa kama Bensoul, Kristoff,Kundi la Kaskazini.

Nviiri amesema kwamba kabla apatane na kundi la Sauti Sol alipata wakati mgumu kufadhili kazi yake ya sanaa.

"Sikuwa na hela ya kuufanya muziki. Nilikuwa na kipaji cha kucheza gitaa. Kama sio kujituma bado ningekuwa videographer."

Nviiri ni kitindamimba katika familia ya watoto wawili.

Soma hadithi nyingine hapa:

"Mtoto wa pili.Tuko wawili kwa famila yetu."

Safari ya muziki haijakuwa rahisi kwa staa huyu

"Muziki inahitaji uvumilivu..Nmekaa kwa miaka 8 bila kusikika."

Nviiri alisema kuwa uoga wa iwapo utakubalika ulimwingia baada ya kutoa ngoma na ikawa kubwa.

"Presha iko kwamba lazima uanze kufanya kazi...Tena ujitume na kuitunza kazi.'