NYAHUNYO: Mpenzi 'wetu' Alikuwa Anatuanikia Nanga Halafu Anatuibia

Jameni swala la mapenzi nikama limegeuka kuwa mchezo wa kadanda kwani kulingana na jamaa kwa jina Ondari, yeye na marafiki zake wawili wana uhusiano wa mapenzi na mwanadada mmoja.

Ondari kutoka Kitale alifichua hili katika kitengo cha Nyahunyo katika kipindi cha Mbusii na Lion teketeke.

Alisema kuwa yeye na wenzake wawili walikuwa na uhusiano na mwanadada mmoja kwa jina Claire ambaye hakuwa na shida yoyote kushiriki kimapenzi nao akijua wazi kuwa wote ni marafiki. Isitoshe baada ya kushiriki nao kimapenzi huwa anawaibia, kuanzia simu za rununu hadi vyombo vya nyumba.

"Claire ana tabia ya kuibia macchali vitu kwani pia mimi aliniibia runinga, simu mpaka blanketi bana." Alisema bwana Odari huku akifichua kuwa hayo yalifanyika wakiwa wapenzi.

"Alipita pia ni vitu za Geoffrey ambaye pia alikuwa anampiga kuni, juzi nayo alimuibia Eric ambaye ni rafiki yangu, dame anatuchapanisha vichwa bana." Alieleza.

Pata uhondo kamili.

&feature=youtu.be