NYAHUNYO: Mwangi Hudanganya Ni Mgonjwa, Nikimdunga Pesa Anatoa Lock Kuruka

Jameni dunia hii ina watu na watu wasioelewa jinsi ya kutumia utu.

Ni ishara tosha kuwa msemo wa 'mwanaume ni effort ' umepotoshwa na kutumiwa isivyokubalika kwani sio wanaume pekee wala pia wanawake wako tayari kutumia ujanja wowote ule ili kujinufaisha kimaisha hata kama sio kulingana na sheria.

 Baadahi ya yale wanayofanya ni kutumia uwongo, kukejeli na pia kutumia wizi wa mabavu ili kujinufaisha na mali ya wenzao.

Kulingana na jamaa kwa jina William, kutoka maeneo ya Githurai 45, Nairobi, jamaa rafiki yake kwa jina 'Mwangi' ana tabia ya kuhadaa wenzake  ili ajipatie riziki.

Alidai kuwa Mwangi ana tabia ya kudanganya marafiki zake kuwa ni mgonjwa maradhi tofauti tofauti huku akidai mchango ili akatibiwe, na mara anapopewa zile fedha anakimbilia pombe huku akidai kuwa alitembelea hospitali na kuwa amepona tayari.

"Mwangi ana tabia mbaya sana Mbusii." Alilalamika bwana William katika kipindi cha Mbusii na Lion Teketeke, kitengo cha Nyahunyo.

" Jamaa anasema ati nimsaidie doh ati amengoja Typhoid nikishamdunga kitu soo mbili hivi jamaa anaenda ulevi anaenda kulewa nazo, anarudi anasema amepona. Sasa hiyo ndio tabia ako nayo nataka mumlime kabisa." Alielezea zaidi bwana William mwenye wingi wa machungu.

Pata uhondo wote katika kanda ifuatayo.