NYAHUNYO: Nina Hamu ya Kumuanikia Lakini Bwanangu Hataki Kunipiga Kuni

Kama kawaida kitengo cha Nyahunyo katika kipindi cha Mbusii na Lion Teketeke ambacho hupeperushwa kila siku ya wiki kuanzia saa tisa alasiri hadi saa moja, vituko, vichekesho na ngoma kabambe ni yale huwezi kosa.

Basi kitengo hiki huwa cha kuwarekebisha watu ambao wamelegeza kamba ifikapo ni maswala ya kukiuka sheria au kukosa tabia njema katika jamii. Katika kitengo hiki, Mbusii na Lion ndio huadhibu waliokosea kwa kuwapiga nyahunyo.

Katika kitengo cha hivi maajuzi, mwanadada mmoja alipiga simu akitaka mumewe anyoroshwe na nyahunyo kisa na maana; Hajakuwa nyumbani tangia mwezi wa Januari. Isitoshe mumewe anaporejea kwa siku moja au mbili, hataki kushiriki mapenzi naye au ukipenda kumpiga kuni, katika lugha ya sheng'.

"Mimi nataka bwana yangu Joseph apigwe nyahunyo." Alisema Irene. "Hataki kuja nyumbani, mara ya mwisho kuja nyumbani ilikuwa Januari siku moja pekee. Sina mwanaume mwingine wa kunishughulikia." Aliongeza mwanadada yule ambaye pamoja na Joseph wana mtoto moja.

Pata uhondo kamili katika kanda ifuatayo.

&feature=youtu.be