'Nyimbo za mapenzi husaidia kuendeleza maisha,' - Jah Cure

Jah Cure ambaye ni mwimbaji wa Jamica yumo nchini Kenya. Atakuwa na maonyesho katika Bustani za Uhuru leo jioni.
Hii ni mara ya pili nyota huyo aiimba hapa Kenya.

"Naipenda Kenya na nadhani nina uhusiano na Wakenya," Jah Cure aliwaambia waandishi wa habari jana.

Jah Cure anajulikana kama mfalme wa nyimba za Rock na Reggae Roots. Anasema anaimba nyimbo za mapenzi kwa sababu zinasaidia kujenga maisha zaidi.
"Niligundua kwamba nyimbo za mapenzi hujenga maisha na nimezingatia kuimba zaidi," Jah alisema.
Jah Cure anasema kuwa anafuraha kwani ataweza kuzungumza na watu wa ghetto na kuweza kutembea kule kibera kuwaona watu wake.
Aliongezea na kusema atakuwa anawatembelea wamaasai na kuvaa nguo wanazozivaa.
"Nitaziimba nyimbo mnazozijua na zile ambazo mtaagiza,"alisema.
Umoja Splash Festival inalenga kukuza umoja miongini mwa vijana.