Nyota wa filamu Idris Elba apatikana na virusi vya Corona

idris Elba
idris Elba
Muigizaji maarufu wa fialamu na msanii wa muziki  muingereza  Idrissa Akuna Elba al maarufu  Idris Elba  ndiye mtu wa hivi punde maarufu kupatikana   na virusi vya corona .

Katika video aliyoweka mtandaoni ,akiwa pamoja na mkewe Sabrina Dhowre,  Elba amesema alipimwa na kupatikana na virusi hivyo. Hata hivyo amewatuliza mashabiki  wake akisema hana  daalili za ugonjwa huo na alijitenga alipogundua  kwamba kuna  uwezakano alitangamana na watu

 Aliandika;

https://twitter.com/idriselba/status/1239617034901524481

Idris Elba  aliendelea kueleza umuhimu watu kunawa mikono  na kuepuka mikutano ya hadhara huku ulimwengu ukiendelea kupambana na mkurupuko wa virusi hivyo .zaidi ya mataifa 30 ya afrika yameripoti visa vya ugonjwa huo  huku kenya  ikisajili visa takriban vinne hadi kufikia sasa