Nyufa zilizopo kati ya ofisi ya Ruto na Uhuru, hafla ya Ruto yawekwa kando

untitled_design_46_11
untitled_design_46_11
Mkutano wa Uhuru Kenyatta na viongozi wa eneo la mlima Kenya umeibua maswala mapya ambayo hayakukusudiwa.

Nyufa zimeonekana waziwazi kuwa huenda ofisi ya Ruto na Uhuru hazina mipangilio mwafaka na zinakosa kushauriana kuhusu mikutano.

Ruto alikuwa na hafla yake Nyeri na kuisitisha baada ya taarifa kuwa Uhuru atakuwa na mkutano Sagana.

Ziara hii imewekwa kando ili kumpisha Rais Kenyatta kufanya kikao na wabunge wa mlima Kenya.

Wachanganuzi wa siasa wanahoji kuwa huenda uhusiano wa karibu uliokuwepo wa viongozi hawa wawili ulikatika ghafla baada ya wandani wa Uhuru kugundua ngome yake inavamiwa na wabunge kugeuza ufuasi wao kwa Ruto.

Mbunge wa Nyeri mjini Ngunjiri amenukuliwa akisema kuwa Ruto ana dhana potovu kuwa anaweza kurithi kura za mlima Kenya bila kuhusisha Uhuru swala na ambalo ni ngumu zaidi.

Mkutano huu ambao umeitwa ili kuzungumzia swala la BBI na kukomesha upinzani katika ngome ya rais umepelekea Ruto kupangua ziara yake.

Viongozi wa chama tawala cha Jubilee kimegawanyika katika makundi mawili, TangaTanga na Kieleweke.

Timu ya TangaTanga ina wandani wa naibu wa rais wanaopinga BBI.

Kieleweke ni kikundi kinachounga mkono BBI na kinadaiwa kuwa kinaunga mkono urafiki wa Raila Odinga na Rais Uhuru Kenyatta.

Ruto alitarajiwa kufika katika hafla ya kuchanga hela katika kanisa la AIPCA Giakanja ,kaunti ya Nyeri.

Hii ni mara ya mwili mwezi huu hafla za Rais na naibu wa rais kugongana.

Siku chache nyuma, Ruto alipangua ziara ya Murang'a baada ya kugundua Uhuru alitarajiwa kutua eneo hilo pia.

Je,unafikiri kwamba kuna mawasiliano mwafaka kati ya ofisi ya Rais na naibu wake?