RC 1

Nyumba na vibanda katika Nairobi Railways club zabomolewa kuruhusu ujenzi wa Nairobi Express Way

Wafanyibiashara  katika eneo la  Nairobi Railways club  wameamkia hasara baada ya biashara zao kubomolewa usiku  . Maamlaka zilitekeleza ubomoaji huo usiku wa kuamkia jumatano baada ya wafanyibiashara hao kupewa notisi ya kuondoka ili kutoa nafasi ya ujenzi wa barabara mpya ya  Nairobi Express Way.

Geoffrey Majiwa aapishwa kama naibu spika wa bunge la Nairobi

Vikosi vya maafisa wa polisi vilikuwa vimepiga kambi katika eneo hilo na ni wafanyikazi wa hoteli pekee walioruhusiwa kuingia ndani .Mkuu mmoja wa polisi alisema maelezo Zaidi kuhusu tukio hilo yangepatikana katika makao makuu ya shirika la Reli .

Pharis Ngotho,  kaimu afisa mkuu mtendaji wa  mpango  mafaai ya kustaafu wa wafanyika wa shirika la Reli  alikuwa ametuma arifa ya kuwashauri wafanyibiashara katika eneo hilo kuondoa bidhaa zao kwa sababu ardhi hiyo ilikuwa inachukuliwa na serikali kwa lazima kufanikisha mradi huo wa barabara .

RC 5

Miongoni mwa walioathiriwa na ubomoaji  huo ni wauzaji wa magari

 RC 2

RC 3

RC 4

 

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments