NZIGE NI FOOD: Msicheze na chakula,Mtaalam aeleza jinsi unavyweza kutayarisha mlo wa Nzige.

nzige.jfif
nzige.jfif
Its Official.Iwapo umekuwa  ukisitasita kuamua iwapo nzige amao wamevamia sehemu nyingi za taifa wanaweza kuliwa ,basi usijisumbu kwa sababu wadudu hao wanaweza kuliwa na ni watam sana .Mtaalam wa Entomolojia Dr.Muo Kasina amesema nzige wana protini muhimu sana na wanaweza kuliwa baada ya kukushwa au kukaangwa .

Anasema taifa linafaa kubadili mtindo wa kushughulikia uvamizi wa wadudu hao  na kuanza kuwatumia kama chakula  kwa sababu huenda wakasambaa na kuyavamia maeneo mengine ya nchi . Nzige hao kwa sasa wamezivamia kaunti za Wajir,Mandera,Isiolo,Garissa na Meru .

Kwanza hakikisha unawatoa miguu na mabawa kasha uwakaushe kwenye pani au kutumia mafuta adimu .unaweza kuongeza  viungo kama vile vitunguu au nyanya ili kuboresha ladha lakini kuwala hivyo kikavu pia ni watamu ,amesema Dr.Muo.Baada ya uvamizi wa nzige katika sehemu za kaskazini mashariki ,kumekuwa na mjadala kuhusu iwapo wadudu hao wanaweza kuliwa .Baadhi ya wakenya wamekuwa wakiogopa kujaribu mlo huo lakini waliotambua umuhimu wa protini tayari walianza safari ya kujitegemea.