Obare aachiliwa kwa dhamana ya laki moja

unnamed (39) (1)
unnamed (39) (1)
Mwanablogu tatanishi wa humu nchini Edgar Obare ameachiliwa kwa dhamana na mahakama ya Kiambu ya shilingi laki moja ama na mdhamini sawia wa shilingi laki tatu baada ya kushtakiwa kwa madai ya kufichua taarifa za siri za mwanamke Natalie Wanjiru Gijithi almaarufu kama Natalie Tewa.

Obare alifikishwa katika mahakama hiyo ya Kiambu mapema Jumatatu na kukana mashtaka dhidi yake ambayo yalikuwa yamewasilishwa na mlalamishi.

Obare aliwasilishwa na mawakili   Titus Munene Kinyua na Ojijo Kepher.

Kesi hiyo sasa inatarajiwa kutajwa mnamo Agosti 21 huku ikirejelewa Novemba 2 mwaka huu.

Ifahamike kuwa Obare alitiwa mbaroni Ijumaa akiwa kaunti ya Kisumu na makachero kutoka DCI ilki kujibu mashtaka yaliyokuwa yanamkumba.