OCS wa Gilgil asherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa sherehe ambao hakuitarajia

unnamed.7
unnamed.7
Wakazi wa Gilgil katika kaunti ya Nakuru waliisherehekea siku ya kuzaliwa ya OCS, Albert Kipchumba, alipokuwa anaadhimisha miaka 43. Wakazi na wenzake wa afisa huyo waliipanga sherehe hiyo bila Kipchumba kujua.

Albert alianza siku yake kama kawaida ya kuwahudumia wakaazi na kufanya doria. Saa 5 jioni alipokea simu kutoka kwa rafiki aliyemwambia mahali ambapo angeweza kuwashika wahalifu.

Niliambiwa kulikuwa na kikundi cha vijana kinachotumia bhangi katika moja ya vilabu. Baada ya kazi, rafiki yangu Wahinya alinichukua na kunipeleka kwenye eneo la tukio

Aliendelea kusema,

Nilikaa kwenye konamoja, na hapo watu walinimwagilia maji zaidi ya lita 200 za maji. Sikuelewa kilichokuwa kikiendelea. Akili yangu ilizunguka sana hadi mmoja wao akasema 'happy birthday' na wote wakaanza kutabasamu.

Kulikuwa na keki na chakula kingi. Rafiki yake Erastus Wahinya, ndiye aliandaa sherehe hiyo.

"Niliratibu na kufanikiwa kumshawishi na akaingia katika mtego. Zaidi ya watu 60 walihudhuria na hakuweza kuamini, "Wahinya alisema.

Waliokuwepo walisifu OCS kwa vile alivyofanya kazi yake ya kutuliza uhalifu katika eneo hilo. Walisema amepunguza ukiukaji wa pombe haramu na mauaji wasichana.

Kipchumba alishukuru kwa sherehe hio. "Sasa najua kuwa nina familia huko Gilgil. Familia yangu iko mbali, kwa hivyo, sikutarajia sherehe kama hio. Nimefurahia zaidi"alisema.

Kipchumba ameonyeshwa kwenye runinga ya kitaifa kwa msimamo wake wa kulinda haki za mtoto wa kike.

Soma mengi