ighalo

Odion Ighalo huenda akashiriki mechi ya United dhidi ya Chelsea

Odion Ighalo ataingia moja kwa moja kwenye kikosi cha soka ya jumatatu usiku dhidi ya Chelsea, licha ya kukosa kambi ya mazoezi ya klabu hio kutokana na hofu za vikwazo vya usafiri.

Mchezaji huyo wa miaka 30 alikamilisha uhamisho uliowashangaza wengi kutoka kwa klabu ya Uchina Shanghai Shenhua mwishoni mwa mwezi Januari lakini hakuelekea Uhispania na kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kutokana na mkurupuko wa corona virus.

Meneja wa United anasema walimwacha Ighalo Uingereza kwani hawakuwa na uhakika ataruhusiwa kuingia tena nchini humo, kwa kuwa alikua amewasili kutoka Uchina wiki mbili awali.

Mabingwa watetezi Gor Mahia watakuwa wanatafuta kujiokoa kutoka kwa kichapo walichopata wikendi iliyopita cha 3-1 dhidi ya Sofapaka, watakapopambana na Western Stima leo huko Kisumu. Kocha Steven Polack amewataka washambulizi wake kujipa motisha kabla ya mechi hio, kwani anawalaumu kwa kukosa nafasi za wazi katika mechi yao dhidi ya Sofapaka.

Polack pia amefichua kua kando na Wellington Ochieng na Philemon Otieno ambao wana majeraha, wachezaji hao wengine watacheza.

Mauricio Pochettino amekiri kwamba angependa kuregea kwenye usimamizi wa ligi ya Primia. Pochettino amemaliza miezi mitatu mbali na tajriba yake ya masuala ya soka.

Hata hivyo ni wazi kwamba anatamani sana kuregelea soka haswa ya Uingereza. Pochettino huenda akaajiriwa na klabu yoyote ya ligi ya Premier kwa kazi yake alipokuwa Tottenham.

Nahodha wa timu ya raga ya Kenya Sevens Rugby Andrew Amonde ataweza kushiriki michuano ya mwezi ujao ya Los Angeles na Vancouver Sevens.

Nilikubali mshahara wangu upunguzwe ili nijiunge na Man United – Ighalo

Hatma ya Amonde ilikuwa huaijulikani baada ya kupata jeraha la goti wakati wa Sydney Sevens lakini baada ya kufanyiwa uchunguzi jumatatu, ikabainika kuwa jeraha hilo sio mbaya na ataweza kucheza mwezi ujao.

Timu hio iliregelea mazoezi jumatatu, inapojitayarisha kwa Los Angeles sevens ambapo watapamba na Afrika Kusini, Canada na Ireland katika kundi B.

 

Kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho mwenye umri wa miaka 27, ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona kwa kitita cha chini ya pauni milioni 77 mwisho wa msimu huu huku Manchester United, Chelsea, Manchester City, Tottenham na Liverpool zote zikimnyatia.

Chelsea inaelekea kumnyakua kipa wa klabu ya Hartlepool na Uingereza Brad Young mwenye umri wa miaka 17, ambaye pia anasakwa na Manchester United na Arsenal.

MICHEZO: Man U yamsajili Ighalo, Shujaa yaanza vibaya mashindano ya Sydney 7s

Wing’a wa Barcelona Ousmane Dembele atasalia nje kwa muda wa miezi 6 baada ya kufanyiwa upasuaji wa paja. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hajacheza tangu Novemba tarehe 27 alipopata jeraha hilo katika kipindi cha kwanza cha mechi yao ya ligi ya mabingwa waliyoshinda 3-1 dhidi ya Borussia Dortmund.

Dembele amekuwa akipata nafuu lakini akalifanya jeraha hilo kuwa baya zaidi wakati wa mazoezi wiki iliyopita. Huenda pia akakosa michuano wa Ufaransa wa Uro mwaka 2020 dhidi ya Ujerumani Juni tarehe.

Dembele alihamia Nou Camp kutoka Dortmund Agosti mwaka 2017 na amefunga mabao 19 katika mechi 74 alizochezea klabu hio.

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments