ODM kuhamia katika makao makuu mapya

abab
abab
Chama cha ODM kitakuwa kinazindua makao makuu yake mpya siku ya alhamisi.

Makao mapya ya chama hicho yatapatikana Lavington mita 300 kutoka kwa makao makuu ya chama cha ANC .

Makao makuu ya chama hicho yamekuwa Kilimani tangu mwaka 2006.

 Philip Etale ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano katika chama cha ODM  amesema kuwa ofisi hiyo sasa inamilikiwa kikamilifu na chama hicho.

Makao makuu ya Kilimani yalikuwa ofisi ya chama cha ODM hadi  wakati chama hicho hakikuwa na makubaliano na mmiliki wa mali hiyo Caroli Omondi ambaye alikuwa msaidizi wa Raila.

Wakati wa uzinduzi wa makao makuu, chama hicho pia kitazindua mpango wake wa usajili wa wanachama kupitia mfumo wa kidigitali.