ODM yateua jopo la kurahisisha mapendekezo ya BBI

Screenshot_from_2019_12_10_11_33_01__1575966900_59386
Screenshot_from_2019_12_10_11_33_01__1575966900_59386
Chama cha ODM kimeteua jopo la kurahisisha mapendekezo ya BBI katika lugha inayoeleweka kwa urahisi na wananchi.

Jopo hili linahusisha mawakili wakuu ,wasomi ,washikadau na viongozi wa vyama vya kisiasa.

Ripoti ya kurasa 156 itawekwa katika lugha nyepesi kwa mwananchi wa kawaida.

Hatua hii imechukuliwa kwani jinsi ilivyo ripoti hii haiwezi kueleweka vyema na imejaa vifungu vya kisheria.https://radiojambo.co.ke/kamanda-wa-alshabab-katika-shambulizi-la-basi-wajir-alikuwa-mwalimu-mkuu/

Jopo hili tayari lishaanza kazi na linatarajiwa kumaliza mwisho wa mwaka huu.

Hii itafungua nafasi ya kufanya misafara ya kisiasa kue200406-2lezea wananchi kuhusu ripoti hiyo.

“Kikosi hiki kitaweka BBI katika lugha rahisi na inayoeleweka na watu wote, hususan wanachama wetu,' Chanzo kutoka Orange House kilismulia gazeti la The Star.

“Tukona kikosi ambacho kinarahisisha mapendekezo ya BBI..." Alisema Mbadi kwenye mahojiano ya simu.