bkvurvspizqtsxs584134b698c9a__1573988161_95746

ODM yatoa kauli kuhusiana na mkutano uliofanyika Sagana IJumaa

Chama cha ODM kimemsifia sana Rais Uhuru Kenyatta kuhusu tamko lake kuhusu lengo la BBI katika mkutano uliofanyika Sagana.

Aidha, mwenyekiti wa ODM amesema kuwa Uhuru anathamini sana ‘Handshake’ iliyofanyika kati ya Raila Odinga na Uhuru Kenyatta.

(+ Picha )Mke wa Mwanahabari Richard Muema aliyepigwa risasi Kasarani afunguka

Kupitia kauli iliyochapishwa leo Jumapili, ODM inaona msimamo dhabiti wa Uhuru Kenyatta katika juhudi za kuunganisha Taifa la Kenya.

Mbadi amesema kuwa alifuatilia kwa makini kilichoenedelea katika mkutano wa Sagana.

 Katika mkutano huo wa Ijumaa, Rais aliwaonya wanaopinga BBI hata kabla hawajapata nafasi ya kuiona.

Uhuru alisisitiza kuwa BBI na ‘Handshake’ zina umuhimu mkubwa wa kuleta amani Kenya na wala haipangi mipango yoyote ya siasa za 2022.

Mkutano huu wa pili wa Rais Kenyatta ulilenga kuziba nyufa zilizosababishwa na vikundi vya TangaTanga na Kieleweke.

Aidha, ODM imesema Rais alifurahishwa na uchaguzi mdogo uliofanyika Kibra Novemba 7,

Aliyetekwa nyara’ apatikana na mpenzi akijipa raha Thika Road Mall, DCI yaeleza

“Katika miaka yangu yote sijawai ona kampeni ya amani Kibra. Kuna baadhi ya watu wachache walirushiwa mawe lakini hatukuona duka likichomwa au watu wakiwa na wakati mgumu wakienda nyumbani,” Uhuru alisema.

“Iwapo uchaguzi unaweza ukafanywa Kibra na watu hawatapoteza mali yao au maisha yao basi hiyo ni ushindi na watu wanafaa kujifunza kutokana na hilo.” Uhuru.

Photo Credits: KUMBUKUMBU

Read More:

Comments

comments