ITS OFFICIAL:James Nyoro aapishwa kuwa Gavana wa Kiambu .

Nyoro
Nyoro
Kaunti ya Kiambu sasa ina gavana mpya baada ya James Nyoro kuapishwa leo ili kuichukua nafasi ya Ferdidand Waititu  ambaye  bunge la senate lilipitisha hoja ya kumwondoa afisini siku ya jumatano .Katika hafla ya kufana iliyoandaliwa kwenye makao makuu ya  kaunti hiyo  Nyoro alikula kiapo cha kuchukua wadhfa huo huku akishangiliwa na wafuasi wake .

Nyoro sasa ni gavana wa tatu kuhudumu katika kaunti hiyo chini ya katiba mpya .  Usalama uliimarishwa katika makao makuu ya kaunti hiyo kabla ya hafla ya kumuapisha Nyoro kuanza . wageni walioalikwa walikuwa wameketi katika jukwa la hafla kufikia  saa sita mchana .

Kwingineko  juhudi za gavana wa zamani Ferdinand Waititu  kuzuia kuandaliwa kwa  hafla ya kumuapisha Nyoro zilitumbukia baada ya mahakama kuu kukataa kuzuia   shughuli hiyo . Jaji  Weldon Korir  ameshikilia kwamba pande zote zinafaa kufika mbele ya jaji James Makau siku ya jumatatu  kwa  kikao cha kusikiliza mawasilisho kutoka pande zote .