Oh no!Bodaboda Mbakaji akamatwa baada ya kumfanyia unyama mteja na kumuacha kileleshwa

Boda boda
Boda boda
Mhudumu mmoja wa bodaboda  wa kampuni ya kutisha huduma za usafiri kutumia mfumo wa simu amekamatwa siku ya alhamisi  usiku na maafisa wa DCI baada ya kumwibia ,kumbaka na kumuacha mteja wake .

Mshukiwa aliyetambuliwa kama Dennis Wekesa mwenye umri wa miaka 27  alimfanyia unyama huyo mwanamke mzungu kabla ya kutoroka na vifaa vyake na  kumuacha katika  kichochoro kimoja . Mwathiriwa alikuwa ameitisha huduma za pikipiki kwenda mtaani kileleshwa katika   jumba la  Anahita Appartments  eneo la parkalands .

" Walipokuwa wakienda parklands ,mhudumu wa  boda boda  alishuka na kumbaka mteja wake na kisha kumpokonya kila kitu na kuizima simu yake’ DCI imsema

Alikamatwa na maafisa wa ktengo maalum cha kuzuia uhalifu katika eneo la Gachie . Mwathiriwa  amehsapokea matibabu hospitalini na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Wekesa atafikishwa kortini  pindi uchunguzi wa tukio hilo utakapokamilishwa.