Siku ya Jumanne tarehe 31, rais wa Uganda Yoweri Museveni alitangaza visa 11 vipya vya ugonjwa huo na kufikisha jumla ya watu 44 walioambukizwa COVID 19 nchini Uganda. 11 hao ni pamoja na watoto 5 wa kwaya hiyo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na kwaya hiyo, makundi yao mawili yalirejea kutoka Marekani na Canada wiki mbili zilizopita. Kwaya zote mbili kisha ziliwekwa chini ya karantini baada ya kuwasili Uganda tangu machi tarehe 20 .
“ Mtu mmoja mzima alipatikana na virusi hivyo wakati huo na mara moja akatengwa’ sehemu ya taarifa hiyo inasema .
Baada ya wengine kupimwa, watu watatu wazima na mtoto mmoja walipatikana na virusi hivyo na kulazimisha vipimo kufanywa kwa wanachama wote waliosafiri. Kwaya hiyo imekuwa ikifanya ziara za matiafa ya nje imezuru Marekani, Canada na Uingereza. Uganda imetangaza marufuku ya kutotoka nje kwa muda wa wiki mbili ili kuzuia usambaaji wa virusi hivyo na kufunga mipaka yake .