Okiya Omtatah ashinda kesi na kurejesha ardi ya umma

Okiya Omtatah
Okiya Omtatah
Mwanaharakati Okiya Omutata, siku ya Jumanne alishinda kesi ambapo alitaka kipande cha ardhi ya serikali kilichokuwa kimenyakuliwa katika eneo la Nasewa, eneo bunge la Matayos kaunti ya Busia kurejeshwa kwa umma.

Kupitia twitter siku ya Ijumuaa, mwanaharakati huo, alifichua kwamba imechukuwa miaka minane ya vuta ni kuvute kortini na nje kurejesha jumla ya ekari 843 za ardhi kutoka kampuni ya Busia Sugar.

Omtata alisema kwamba msajili mkuu wa ardhi katika kaunti ya Busia alifutilia mbali cheti cha kumiliki ardhi hiyo kilichokuwa kimetolewa kwa njia ya ulaghai na kutoa cheti kipya kwa Katibu kwa kudumu wa fedha ambaye ndiye mhifadhi wa mali zote za serikali.

Siku ya Ijumaa Omtata alimkabidhi kamishna wa kaunti ya Busia cheti hicho na sasa kitawasilishwa kwa katibu wa kudumu wa fedha.

"Namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuafikia hatua hii," alisema.

Mahakama iliamua kwamba lilikuwa kosa kwa ardhi iliotolewa na wakaazi kwa serikali kupewa kampuni ya kibinafsi.

Serikali ilipata ardhi hiyo kutoka kwa wenyeji wa eneo la Nasewa miaka ya tisini na kuikabidhi kampuni ya kibinafsi kujenga kiwanda.