Oliech arejea tena kabla ya mchuano wa Caf champions League

Aliyekuwa nahodha wa Harambee stars, Dennis Oliech amejumuishwa kwenye kikosi kitakacho shiriki mechi ya maondoano ya klabu bingwa barani Afrika.

Gor Mahia itachuana na mabingwa wa burundi Aigle Noir kwenye mechi ya mkondo wa kwanza tarehe 11 mwezi agosti mjini Bujumbura.

Kwenye kikosi hicho kinachotarajiwa kuongozwa na naibu mkufunzi Patrick Odhiambo kimewajumuisha washambulizi wapya akiwamo Dickson Ambundo na Francis Afriyie.

 Walindalango :Fredrick Odhiambo, David Mapigano, Boniface Oluoch

walinzi: Wellington Ochieng, Philemon Otieno, Shafik Batambuze, Geoffrey Ochieng, Joachim Oluoch, Joash Onyango, Charles Momanyi, Maurice Ojwang.

Viungo: Ernest Wendo, Tobias Otieno, Kenneth Muguna, Curtis Wekesa, Boniface Omondi, Lawrence Juma, Samuel Onyango.

washambulizi: Dennis Oliech, Nicholas Kipkirui, Dickson Ambundo, Gislain Yikpe Gnamien, Francis Afriyie.