Oparanya,Wamalwa wamewarai MCAs kutupilia mbali miswada ya kuwatimua magavana

Mwenyekiti wa baraza la magavana nchini Wycliffe Oparanya na waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa sasa wanataka wawakilishi wadi kutupilia mbali miswada ya kuwatimua magavana nchini.

Akizungumza katika kongamano na wanahabari hii leo, Oparanya amesema kuwa ni sharti wawakilishi hao wasaidiane na magavana ili kuweka mikakati ya kupigana na virusi vya corona.

“Counties don’t have money, the little we have is meant for other priorities, we have already requested the president to give us supplementary budget of five billion shilings,” “Now what are saying is that all these monies MCAs are spending in hiring lawyers, why can’t we use them to buy PPE tests and expansion of bed capacity,” Oparanya .

Kwa upande wake waziri Wamalwa amesema ni vyema idara zote katika majimbo yote 47 kushirikiana ili kutatua mizozo ya uongozi inayoshuhudiwa.

“We want to request MCAs during this pandemic season that we first deal with this situation, we are resilience country, and we’ve dealt with so many disastrous thus appealing them to focus their energy and resources towards this enemy,” Wamalwa a

 Wamalwa amesema kuwa huku maambukizi ya corona yakitarajiwa kuongezeka nchini kati ya mwezi wa Julai na Agosti, ni sharti viongozi katika majimbo yote nchini kuungana ili kutathmini namna ya kuimarisha sekta ya afya nchini.