Licha ya kumpiga kura rais Uhuru Kenyatta katika chaguzi mbili kuu sasa wameanza kuzingatia uwezakano wa kufanya ushirikiano na vyama vingine endapo rais Uhuru Kenyatta hatomuunga mkono Ruto kuwania urais mwaka wa 2022 .
Baadhi ya wabunge kutoka Nandi wakiongozw ana mbunge wa Chesumei Wilson Kogo, wametamaushwa na hatua ya kuondolewa kwa washirika wa Ruto katika nyadhifa za uongozi katika senate .
Seneta wa Elgeyo marakwet Kipchumba Murkomen alifurushwa kama kiongozi wa wengi katika senate ilhali Susan Kihika alionyeshwa mlango kiranja wa wengi kabla ya Kindiki Kithure kuvuliwa madaraka kama naibu spika wa senate .Kogo wamesema hawapingi jitihada za kuleta umoja nchini lakini wanapinga njama za kumzuia Ruto kuchukua usukani wakati rais Uhuru Kenyatta atakapostaafu mwaka wa 2022.
Kogo na mwenyekiti wa kamati ya amani ya Kisumu- Nandi d Kisumu-Nandi Charles Tanui wamesema masaibu ya Ruto yamesababishwa na watu wenye ushawishi mkubwa katika afisi ya rais ambao hawamtaki Ruto kumrithiri Uhuru .