Wairimu

Orodha ya mali 10 inayomilikiwa na mjane Sarah Wairimu

Sarah Wairimu ambaye ni mjane wa bwenyenye Mholanzi Tob Cohen anamiliki mali angalau 10 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 9.

Aliorodhesha mali hiyo kama sehemu ya mahitaji ya korti ili kudhibitisha kuwa ataweza kujikimu baada ya kuachiliwa kwa dhamana.

‘Tongozeni Kina Dada Kwa Heshima Na Utaratibu,’ Uhuru

Hata hivyo Sarah Wairimu haruhusiwi na mahakama kutia guu lake kwenye makaazi ya Kitisuru yenye thamani ya shilingi milioni 400 anayopigania kumiliki baada ya kifo cha mumewe.

Mnamo Ijumaa Wairimu alichaliwa kwa dhamana ya shilingi milioni  baada  kuweka hati ya kiapo kwamba angeweza kujikimu.

Alisema amekuwa akifanya kazi katika maisha yake na katika kipindi hicho amehifadhi akiba ambayo inaweza kukimu mahitaji yake.

Asilimilia 98 Ya Ajali Barabarani Yasababishwa Na Makosa Ya Binadamu
“Nimepata mali ifuatayo ambayo imeandikishwa katika jina langu mimi binafsi kwa wakati fulani na pia nyingine imeandikishwa kwa jina langu pamoja na marafiki na familia yangu,” alisema katika hati ya kiapo.

Yafuatayo ni mali yake  aliyoorodhesha:

• Mahiga / Kihome / 1033 yenye thamani ya Sh1 milioni

• Mahiga / Kihome / 1705 yenye thamani ya Sh1.6 milioni

• KJD / Ntashart / 9072 yenye thamani ya Sh300,000, inamilikiwa kwa pamoja na Renee Gathoni.

• Kajiado / Kitengela / 13364 yenye thamani ya Sh2.5 milioni

• KJD / Ntashart / 10917 yenye thamani ya Sh259,000

• Dundori / Mugwathi Block 1/322 yenye thamani ya Sh4 milioni

• Mpango wa makazi ya Kibwezi Mukaange P / NO 2271 yenye thamani ya Sh595,000

• Vitalu vya Dundori / Mugwathi 1/351, Dundori / Mugwathi Block 1/2822 na Nyeri / Municipality Block ambayo thamani yake haikufafanuliwa.

Picha za siku: Bingwa Eliud Kipchoge awasili nchini

Wairimu pia ameeleza kuwa ana familia na marafiki, akiwemo Mama mmoja Lucy Mwangi ambaye amekubali kumpa makao nyumbani kwake wakati  kesi hiyo inapoendelea.

Jaji Stella Mutuku mnamo Ijumaa aliamuru na kumwonya  Wairimu  dhidi ya kuwasiliana na nduguze wawili wa Cohen .

Photo Credits: Bernard Kigen

Read More:

Comments

comments