Orodha ya mikwaju 5 inayotikisa YouTube. Sautisol, Diamond na Ringtone wapo

Diamond-Platnumz
Diamond-Platnumz
Hii leo tunakusogezea nyimbo 5 bora zinazojizolea nafasi kubwa katika trends za YouTube. Ngoma kupata nafasi hizi za kwanza ni jambo muhali sana. Ni bidii ya kila staa wa muziki au mtunzi wa sanaa yoyote kuona miziki inapata nafasi kama hiyo.

Hapa nakusogezea Orodha ya mikwaju hii. Ikumbukwe kuwa nafasi zilizoshika katika mtandao wa YouTube hubadilika mara kwa mara. Hii inategemea na jinsi watu wanavyotazama katika mtandao huu.

Soma hadithi nyingine:

1. Nandy Ft. Sauti Sol

Ngoma hii inatambulikana kama Kiza Kinene. Staa na nyota wa Tanzania Nandy amewashirikisha kundi la Sauti Sol.

2. Innos'B Ft Diamond Platnumz

Hili ni ligoma la staa na fundi wa muziki Afrika Diamond Platnumz linalokwenda kwa jina Yope Remix akimshirikisha staa wa Kongo Innos’B. Ndani ya masaa 24, mkwaju huu sasa umegonga views Milioni moja na ushei.

Soma hadithi nyingine:

3. Rose Muhando Ft. Ringtone

Jamaa wa skendo Ringtone amedondosha hii Hit Walionicheka akiwa na Rose Muhando.

Soma hadithi nyingine:

4. Aslay Ft.Alikiba

Mastaa hawa wawili wa bongo wamefanya kazi inayoitwa Bembea. Aslay anajitahidi sana kujikaza baada ya kuona Mbosso waliokuwepo bendi moja anajituma zaidi.

5. Rayvanny Ft.Nora Fatehi

Nora medondosha kionjesho cha kazi yake na Rayvanny inayosubiriwa kutoka hivi karibuni.

Mhariri: Davis Ojiambo