Orodha ya vitu ambavyo hukujua kumhusu McDonald Mariga

McDonald Mariga Wanyama, ni mmoja wapo wa wana kandanda waliotajika humu kenya na nchi nyingi za ng'ambo kwa ujuzi wake wa kucheza mpira wa miguu.

Jamaa huyu aliweza kuiweka nchi yetu juu sana kwenye sekta ya mpira wa kandanda alipokuwa akicheza mpira wa miguu. Zaidi ya hayo, jamaa huyu, alikuwa mkenya wa kwanza kabisa kushinda tuzo lililotamaniwa sana na watu, kikombe cha mshindi wa mabingwa ya ligi ya Uefa mwaka wa elfu mbili na kumi.

Amini Usiamini, Mariga ni mgombea wa kiti cha ubunge wa chama cha Jubilee, baada ya kifo cha hayati Ken Okoth.

Zaidi ya hayo, Mariga aliweza kupata alama za juu zaidi katika mahojiano ya uteuzi ya jubilee.

Mariga ni mtu msiri kwani hapendi mambo yake yajulikane sana. Hata hivyo, Radio Jambo imewaandalia mambo ambayo hamkujua kumhusu.

Soma ujue mengi!

1.Mheshimiwa Mariga alizaliwa tarehe nne, mwezi wa nne, mwaka wa elfu moja, mia tisa themanini na saba (1987). Kwa Sasa, shujaa huyu ana miaka thelathini na mbili (32).

2.McDonald ni kifungua mimba wa Mzee Noah Wanyama ambaye pia ni mtu apendaye mpira sana.

3.Ni ndugu yake mkubwa, mchezaji hodari wa timu ya Tottenham Hotspur bwana Victor Wanyama.

4. Alizaliwa katika familia ya watu wanaopenda michezo kwani dada zake hucheza mpira wa vikapu (basketball) na mpira wa wavu (netball). Licha ya hayo, ndugu zake wawili wa kiume ni wanakandanda na wazazi wao pia walikuwa watu wanaopenda michezo.

5.Mariga ameishi kwenye kijiji kidogo cha Muthurwa pamoja na familia yake.

6.Alisomea katika shule ya upili ya Kamunji pamoja na wanakandanda kama Dennis Oliech.

7.Alikuwa mchezaji wa timu kama Ulinzi FC, Tusker na Kenya Pipeline kabla ya kuenda Ulaya.

8.Mwaka wa elfu mbili na tano, Mariga alienda nchi ya Sweden ambapo alichezea Enkopings kwa muda kisha akaenda Helsingborgs.

9.Mariga ni baba ya mtoto mmoja .

10.Ni mwanasiasa.

11.Anagombea kiti cha ubunge wa Kibra.

12.Mc Donald ana mali nyingi sana.

13.Mariga ni baadhi ya watu wa kwanza nchini kenya kuwa na gari aina ya Hammer.

Jamaaa huyu, anaonekana kuwa na mali nyingi sana kutokana na maisha ambayo anaishi. Mgombea wa kiti cha ubunge wa mtaa wa kibra, anaishi kwenye mtaa wa Lavington.Mtaa ambao mabwenyenye huishi. Mariga ana magari,nyumba,saa,na hata pia nguo za hali ya juu sana.