Orodha ya wasanii wa nyimbo za injili ambao walipeana talaka

Neno msanii wa nyimbo za injili linapokuja katika akili za watu, wengi wanatarajia wawe mfano mwema kwa mashabiki kwa kuonyesha mwelekeo mwema kwa watu wengi kwa maana wao wanafahamika sana.

Si wote wanaweza kuonyesha mfano mwema kwa maana kama  kuvumilia kwa  ndoa ambazo zinakumbwa na changamoto si haba.

Miongoni mwa  wasanii hao waliotalakiana na wapenzi wao ni kama ifwatavyo.

1.Joan Wairimu

Kando na uimbaji wake mahiri,Wairimu ni mhubiri maarufu .

Katika ndoa yake ya miaka 7,Wairimu alipitaia katika changamoto si hapa licha ya kuolewa kwa mtu maarufu askofu Mwangangi ambaye alitalakiana naye.

2. Gloria Muliro

Ni msanii ambaye walipeana talaka na mumewe Eric Omba, hatua ambayo Gloria alidai kuwa mumewe Omba alikuwa kikuu na njia kwenye ndoa yao.

3.Betty Bayo

Alikuwa ameolewa na muhubiri Kanyari ambaye alifahamika sana kwa kufanya miujiza,waliachana baada ya mumewe kufichuliwa kufanya miujiza ya uongo katika makala spesheli yaliopeperushwa kwenye mojawapo ya televisheni za humu nchini.

Betty alijulikana baada ya wimbo wake wa '11th hour' kuenea sana.

4.Eunice Njeri

Aliachana na aliyekuwa mumewe mwaka wa 2016 muda mchache baada ya harusi yao.

Eunice ni mwimbaji maarufu na anajulikana kwa kutoa nyimbo zake zinazowapendeza wengi.

na kubadilisha maisha ya wengi sana.

5.Winnie Rose Wangui

Mbali na kazi yake ya usanii ni mtangazaji wa runinga moja humu nchini,akiwa katika mahojiano katika mtandao wakijamii, Winnie alisema ndoa yake ilivunjika baada ya siku chache.

6.Loise Kim

Loise ambaye anapanga kuwania kiti katika uchaguzi ujao, alitengana na mume wake baada ya miezi saba katika ndoa.

Aliimba wimbo wake kwa lugha ya kikuyu ambao unafahamika kama'wedo wa kiabiriria' yaani upendo wa kwanza na kujulikana sana.