Baadhi ya wasanii waliojipata pabaya baada ya madai kuwa wamo na mgogoro au kupatikana kwa njia isiyostahili ni;
1.Ringtone Apoko
Apoko amekuwa kwenye vichwa vya habari mara kwa mara baada ya kupatikana upande usiostahili au kwa mambo yote mabaya.
Mwaka jana Ringtone alionekana kwenye mitandao ya kijamii akiwa amebeba bango la kumtafuta bibi ambapo si jambo njema hasa kwa msanii wa nyimbo za injili.
2.Bahati
Bahati amekuwa kwenye tasnia ya usanii kwa zaidi ya miaka mitano huku akifungua lebo yake iliyokuwa inafahamika kama EMB, kwa muda msanii huyo amekuwa kwenye mitandao ya kijamii wakizozana na wasanii wenzake
Huku kashfa ya kukamatwa kwake msanii Peter Blessings na aliyekuwa produca wake Paulo ikigonga vichwa vya habari kisha mengi kusemwa.
Msanii huyo pia ana Baby mama licha ya kumuoa Diana Marua, hivi sasa ndoa inaendelea vyema.
3. DK Kwenye beat
JIna lake lilifahamika na kufahamika sana wakati alidaiwa kumuambukiza msichana wa kutoka Nakuru na ugonjwa, msanii huyo alikubali makosa au madai hayo na kisha kuomba msamaha.
4.Weezdom
Alienea sana kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha zake na mwanamke mmoja wakiwa kitandani kuibuka kwenye mitandao hiyo,mwanamke huyo alidaiwa kuwa wa msanii mwenzake.
Picha za wawili hao zilionekana walikuwa na mahabara ya mapenzi, kitandani.
5.Hope Kid
Kama vile msanii DK alishtakiwa kuambukiza msichana ugonjwa baada ya kufanya ngono naye, pia msanii Hope kid alikuwa kwenye kashfa hiyo ya msichana huyo huku akiwekwa ndani.
Baadaye Hope kid alikubali makosa yake na kuomba msamaha.
6.Niccah the queen
Wazungu walisema methali hii'my dress my choice' msanii huyo mara kwa mara mavazi yake uwaacha wengi na maswali mengi huku madai ya kuwa kitandani na msanii Weezdom ikigonga vichwa vya habari.
7.Eko dydda
Uvumi ulienea sana kwenye enz zile kuwa msanii huyo amechana na mke wake, huku mkewe akidai mumewe si mwaminifu katika ndoa yao.
Kama msanii mmoja anapaswa kufanya nini ili kujitenga na kashfa tofauti hasa za ngono, ni kweli kila mmoja wetu ni binadamu na lazima tuwe na hisia lakini hisia nyingi zimefanya wasanii wengi kujipata pabaya.
Huku wengi wakilala korokoroni kwa ajili ya madai tofauti, kutokana na uchunguzi wangu wasanii wengi hutaka kutambulika sana huku ikiwabidi wengi kufanya mambo yasiyostahili na mambo hayo kufanya wajipate pabaya na muda kuwa ushaapita baada ya kufahamu walichokuwa wanataka kutenda au kufanya.
Je wanapaswa kufanya nini ili kujitenga na mambo kama hayo? Wengi wanapaswa kujipenda jinsi walivyo na kuridhika na chochote wanapata kama mapato ya na riziki yao ya kila siku.
Si wote ambao upenda kujipata mahali pabaya lakini bila kujua wanajipata upande huo huku wengi wakikejeliwa na kukosolewa vikali na wanamitandao na hata wakenya.
Si mmoja au wawili ambao waliwashangaza wengi baada ya habari zao kugonga vyombo vya habari bali baadhi ya wasanii wengi waliwashangaza mashabiki wao.