Orodha ya watu mashuhuri waliofanya kazi kwenye vyumba vya kuifadhi maiti kabla ya kufahamika

Hawakukosea walipo imba na kusema kuwa kazi ni kazi hata chomela bora upate riziki ya kila siku, usemi huo ni wa ukwli kwa baadhi ya watu mashuhuri wa humu nchini, waliofanya kazi katika vyumba vya kuifadhi maiti kabla ya kuwa mashuhuri waka kufahamika na mashabiki wao.

Hii hapa orodha yao;

1.Miracle Baby

Msanii huyo aliwashtua mashabiki wake na wakenya wengi baada ya kusimulia kazi aliokuwa anafanya kabla ya kupata pesa.

Mbali na kufanya vibarua vingi hapa na pale alikuwa mfanyakazi wa chumba cha kuifadhi maiti.

"Mimi mwenyewe nimefanya kazi nyingi duniani nimekuwa mfanyakazi wa chumba cha kuifadhi maiti, nimeosha mili ya wafu."

2.Eric Njoka

Mwanahabari wa runinga ya K24 alichua kuwa huwa anafanya kazi katika chumba cha kuifadhi maiti, amefanya kazi hiyo kwa muda wa zaidi wa miaka 15.

"Nikiona wala kukumbuka jinsi mili ya wafu inakaa huwa ndoto mbaya zilikuwa zinanijia kila mara, lakini hayo yalipita na kuendelea na kazi yangu
Ndio nina kazi nyingine lakini napenda ya kuwa katika chumba chamaiti kwa maana nafanya kazi ambayo wengi hawawezi fanya."

3.King Kafu

Mtangazaji wa redio ya Ghetto anate fahamika kama Nicholas Cheruyoit almaarufu King Kafu amefanya kazi katika vyumba vya kuifadhi maiti lakini hakuwa anaosha mili ya wafu mbali alikuwa anatengenza jeneza za watu ambao wamekufa kabla ya kuwa mtangazaji.