Kazi ya uigizaji si rahisi kama wengi wanavyoona wakiwa mbele ya kamera wakiigiza na kuwafurahisha wengi.
Si mmoja au wawili bali wafahamu waigizaji tofauti humu nchini na hii hapa orodha yao.
1.Pascal Tokodi
Ni muigizaji katika vipindi au filamu tofauti humu nchini, mbali ya uigizaji Pascal pia ni mwanamuziki, kupitia uigizaji wake ametuzwa tuzo tofauti kwa kuwa muigizaji bora.
Tokodi alifahamika sana kupitia kwenye kipindi cha Selina kinachoonyeshwa kwenye runinga ya Maisha Magic East.
2.Brenda Wairimu
Jinsia ya kike haifahamiki sana kwa mambo mengi ilhali Brenda hakujali watakacho sema wala kuongea, ameenea sana katika sekta ya uigizaji huku akiigiza katika kipindi cha Selina, Monica na vipindi vingine tofauti.
3.Mutran Tamim
Mutran Tamim almaarufu Jasiri katika kipindi cha pete anazidi kuenea na kung'aa katika sekta ya uigizaji.
4. Celistine Gachuhi
Alifahamika sana kupitia katika kipindi cha Selina ambaye ni muigizaji wa maana katika kipindi hicho ambaye anafahamika kama Selina.
Mbali na kazi ya uigizaji Selina, hufanya biashara tofauti ili kujikimu,pia ni mkristo ambaye hajaacha njia zake ilhali amezidi kumtumikia Mola.
5.Lupita Nyong'o
Kwa hakika mwanamke huyu amebarikiwa na talanta ya uigizaji tangu zamani huku akiigiza vipindi tofauti hata nje ya Kenya.
6.Nick Mutuma
Mutuma anafahamika na mashabiki wake kupitia vipindi tofauti anavyoigiza, huku akiwaacha wanawake wengi wakimwaga mate na hata kuwakosesha usingizi kwa maumbile yake
7.Gerald Langiri
Ni muigizaji bali na uigizaji ni mzalishaji na mwelekezi wa vipindi au filamu tofauti humu nchini.
8.Sarah Hassan
Alijulikana sana alipokuwa anaigiza kipindi cha Tahidi High kinachoonyeshwa katika runinga ta Citizen.
9.Serah Ndanu
Anajulikana kwa ukakamavu wake katika uigizaji na pia bidii yake, mbali na uigizaji pia ni mtangazaji
10.Naomi Ng'ang'a
Si mmoja au wawili bali ni muigizaj ambaye wengi hummezea mate kwa umaarufu wake katika uigizaji.
11.Brian Ogana
Anafanya yema katika kazi yake ya uigizaji hasa katika kipindi cha Maria