PAMBANA NA HALI YAKO! Wakenya mtandaoni wamkemea Dennis Itumbi baada ya kushambuliwa na polisi

‘The Internet never forgets’- Ni kauli ambayo umeisikia  mara kadhaa   hususan katika matukio ambayo mtu anasema kitu wakati Fulani bila kujua kwamba sikumoja atajutia .Ndio masaibu yaliomfika Dennis Itumbi alipoweka video  mtandaoni akilalamika jinsi polisi 18 walivyomshambulia na kumpa kichapo bila huruma  katika kituo cha polisi cha Kilimani siku ya  Ijumaa tarehe 10. Itumbi anasema alikuwa amekwenda kulichukua gari lake wakati polisi walipomvamia .

“Wamenichapa,  wamenishambulia kweli .yaani polisi 18  wamenipiga makonde …hawa ni watu aina gani ?’“ Kosa langu  lilikuwa kwenda katika kituo cha polisi kuchukua gari langu’ alisema Itumbi .

Lakini watumiaji wa mitandao waliichakura na kutoa  ujumbe ambao Itumbi aliuandika mwaka wa  2016 uliosema :‘ Sheria inawaruhusu polisi  kutumianguvu katika hali Fulani na mahakama kote ulimwenguni zinatambua hilo’. Itumbi alindika ujumbe huo Mei tarehe 23 mwaka wa 2016 .

Masaibu yake hayo yalijiri saa chache tu baada ya mbunge wa Gatundu Kusini moses Kuria pia kukamatwa katika kituo hicho cha polisi kwa kumshabulia mwanadada mmoja .Kupitia akaunti yake ya Twitter Itumbi alisema alifanyiwa matibabu  na alikuwa tayari kurejea katika kituo hicho kuhakikisha kwamba Kuria anaachiliwa huru .