Papa umefanya nini!Uombolezaji wa Wilbroda kwa Papa Shirandula

Kifo huwa kinaumiza mioyo ya watu na kuacha pengo kubwa katika familia, jamaa na hata marafiki, kifo chake Papa Shirandula kiliacha pengo kubwa katika tasnia ya uigizaji na katika familia yake.

Jumamosi,25,Julai Muigizaji mwenzake Jackline Nyaminde almaarufu Wilbroda alinakili ujumbe wenye huzuni mwingi kwenye mitandao yake ya kijamii, huku akimkumbuka Bukeko kwa mazuri ambao amemfanyia na hata miradi ambayo walikuwa wamepanga katika maisha yao ya usoni.

"Leo namuomboleza mwendazake rafiki yangu, muigizaji mwenzangu, mshauri wangu, jirani yangu na shangazi ya mwanangu wiki iliopita masaa kama haya wakati kama huu nlipokea simu ambayo itaishi kwenye nyayo za akili kwa muda mrefu
Nilisimama kwenye duka kubwa(supermarket) nikiwa nmenyamza, singetembea wala kufanya chochote moyo wangu uliumia sana nilienda kwenye gari langu na kulia kwa sauti papa umefanya nini! Papa umefanya nini!

Tulikuwa na mipango mingi na ya maana, kwa tasnia ya uigizaji tulikuwa hata tumeanza mipango yetu wiki mbili kabla ya kifo chako

Na tulikuwa na wakati mwema pamoja, ulikuwa na furaha na matumaini, miezi hizi tatu tumekuwa marafiki wa karibu sana, tulikaa pamoja, tukala pamoja na hata kucheka pamoja

Hamna kitu chochote kilikuwa kimeni tayarisha kwa kifo chako, sijawahi hisi kudanganywa hivi maishani mwangu, nimepata pigo kubwa duniani lakini kifo chako ni pigo kubwa sana

Uliaga dunia hivo tu, nilikuwa nawe jumanne na tukazungumza, ijumaa jioni ulikuwa na mtotot wangu na mliongea lakini jumamosi haukuwa nasi tena." Aliandika Wilbroda.

Hizi hapa baadhi za jumbe za mashabiki wake Wilbroda;

wanja_tajiri Am deeply sorry for your hurt. May God surround you with peace during this time.

nancynikitah Life is too short, papa was full of life even if you were sad you find yourself laughing while watching his comedy, rest in peace.

kades_kadz Amen. My condolences dear. And may the good Lord receive paps well

everlynepeter It is well with our God🙏

caroltheartem It’s still painful haki

kadacyiah Continue resting papa as your legacy lives…to Him we belong and unto Him we shall return

fteyba Forever in our heart 😘

maureenakinyi024 So touching my dear Willbroda😧 take ❤❤