Passaris afanyiwa upasuaji wa mgongo

Mwakilishi wa wanawake wa Nairobi Esither Passaris amefanyiwa upasuaji iliofaulu katika hospitali ya Aga Khan Nairobi.

Passaris alilazwa siku ya Jumatatu baada ya kuhimili maumivu ya mgongo kwa takriban miongo miwili. Alifanyiwa upasuaji spesheli wa mgongo kurekebisha tatizo la neva katika uti wa mgongo (Medial Branch Block procedure).

Passaris kupitia ujumbe wa twitter siku ya Jumanne alisema ulikuwa usiku wa kwanza kulala bila maumivu.

"Namshukuru Mungu kwa upasuaji wangu ulioenda vizuri. Nilikuwa na usiku wangu wa kwanza bila maumivu katika kipindi cha zaidi ya miezi miwili," Passaris alisema na kuongeza kwamba tayari ameanza mazoezi kumwezesha arejelee hali yake ya kawaida.

Aliwashukuru wakenya kwa kumuunga mkono kupitia maombi na salamu zao za heri njema.

Mwezi Februari Passaris alifanyiwa upasuaji kuondoa tezi shingoni mwake ili kutibu uvumbe shingoni.