Pastor (1)

Pastor ashtakiwa kwa kumnajisi msichana kwa miaka tatu!

Je huu ni ungwana?

Pastor (1)

Mhubiri mmoja wa kanisa la African Divine Church, ashtakiwa kwa kumnajisi msichana wa miaka kumi na moja kwa miaka tatu. Binti huyu ambaye tutampa jina Mary, alikuwa akiteseka kimoyomoyo kwani alikuwa anajiona mdogo sana na kwasababu hakuna mtu angeamini anachosema endapo angefunguka na kusema yanayofanyika.

Binti Mary, ambaye anaishi na nyanya yake, alifunguka na kusema kuwa, mara ya kwanza kunajisiwa na Pastor Ambani, alikuwa ameshtuka sana na hata akawa na mawazo chungu nzima.

Akilini mwake, alikuwa anafikiri kuwa hakuna mtu atakaye amini Pastor anaweza fanya kitendo cha kinyama hivyo, kwani mhubiri huyu alikuwa anahubiri kuhusu mambo ya utukufu wa bwana kila jumapili kanisani.

Katika mashtaka kortini, Bwana Ambani alikataa madai hayo na amekaa kwenye rumande kwa mwezi mmoja kwani ameshindwa kulipa dhamana ya elfu mia tatu.

Mary alimwambia hakimu wa korti za kibera, bwana Barbara Ojoo kuwa yote yalianza mwaka wa elfu mbili kumi na tano ambapo, Pastor Ambani alienda kwenye nyumba ya nyanya yake alipokuwa akiishi Mary na kusema kuwa anataka kutazama kipindi.

Niko tayari kujaza nafasi ya Ken Okoth – Eliud Owalo

Zaidi ya hayo, Pastor Ambani alibisha mlango na Mary alipofungua, aliuliza kama nyanya yake yuko na aliposema hayuko, akaomba kukaa kwenye nyumba hiyo na kuomba ruhusa ya kutizama sinema.

 “He knocked on the door and when I opened it, he asked if my grandmother was in. When I told him that I was alone, he got in, sat on a chair and asked me to allow him to watch a movie.” Mary said.

Baada ya dakika chache, Mary alisema kuwa, Pastor alitoka kwenye kiti chake na kukaa karibu naye .

“He held my shoulder and asked me to relax with him.

Vilevile, alikuwa ameshtuka lakini hakuna kitu chochote aliweza kufanya kwani alikuwa anajiambia akilini kuwa, bwana huyu ni pastor na kwa hivyo hawezi jaribu kufanya mambo yasiyofaa.

“I was shocked but I did nothing because he is a pastor. All he wanted was to relax, I thought in my head,” alisema.

Hata hivyo, alijua kuwa bwana huyu alikuwa ametoa mavazi yake ya kanisani na kugeukia kondoo wake alipoanza kumshika kimwili.

Jinsi punda wanavyo watajirisha wachuuzi wa maji mtaani Rongai, Kajiado

“He touched my chest and lifted me up onto his lap where he continued caressing me. I was totally confused and scared,” alisema.

Ambani aliendelea na kitendo hicho cha kumnajisi kisha akampa chips za shilingi hamsini na kumwambia asiambie mtu yeyote.

Zaidi ya hayo, Ambani alisisitiza na kusema kuwa, baada ya siku hiyo ya kwanza, Ambani alizidi kuenda katika nyumba hiyo na kumnajisi kila wakati na nyakati zingine, kumlazimisha binti huyu aende kwake na kumnajisi pia.

Tabia hii iliendelea kwa miaka mitatu na kila mara alipomwambia Ambani anaumia, bwana huyu angemcheka.

Walipokuwa kortini, nyanyake Mary alisema kuwa majirani walikuwa wanamuonya na kumwambia kuwa wanashuku kuwa Pastor humnajisi Mary na alipomuuliza Mary, hapo ndipo alifunguka na kusema ukweli.

“My neighbour told me that he saw the accused person leaving my house several times and said they suspected that he was defiling my grandchild. I asked Mary and she confirmed that she was indeed being abused,” alisema.

Ama kwa hakika, lisemwalo lipo na kama halipo, laja.

Mwanamke huyu alimpeleka Mary hospitali ya Nairobi Women alipopata matibabu na akakaza mwendo mpaka kwenye kituo cha polisi cha Kabete kisha Ambani akatiwa mbaroni.

Ambani alimuomba hakimu aishukishe dhamana yake kwani, amekaa kwenye rumande kwa mwezi mmoja kwa sababu ya kushindwa kupata pesa hizo .

Hata hivyo, Bwana Ojoo alikata ombi  hilo na kusema kuwa, kesi yake itaskizwa mwezi ujao.

 

Photo Credits: The Star

Read More:

Comments

comments