Pata kujua jinsi Harambee stars watafuzu karika raundi ya 16 bora

harambee-stars
harambee-stars
Baada ya kucharazwa 3-0 na senagal, Wakenya wamekufa moyo ila bado stars wanauwezo wa kutinga hatua ya 16 bora. Hata hivyo, Kenya inahitaji usaidizi kutoka kwa mataifa kadhaa ili iweze kufuzu kwenye hatua ya 16 Bora.

Kenya ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Algeria magoli mawili bila jibu kisha ikamnyuka Tanzania 3-2 na kumalizia udhia na senegal kwa kichapo cha 3-0.

Kwenye hatua ya 16 bora, mataifa kumi na mawili yatafuzu kama nambari moja na mbili mtawalia huku pia kukiwa na mataifa manne yatakayo fuzu kama nambari tatu.

Kenya ilimaliza kundi C katika nafasi ya tatu na hivyo basi kujiweka katika nafasi ya mataifa yanayo nga'nga'nia nafasi nne zilizobaki. Harambee stars ili iweze kufuzu lazima mambo yafuatayo yatokee:

  1. Cameroon wamlaze Benin
  2. Black stars ya Ghana ichape au ichapwe na Guinea-Bissau
  3. Tunisia ilaze Mauritania
  4. Mali ilaze Angola

Iwapo mambo hayo yatatokea basi Kenya itakuwa imefuzu kwenye hatua ya 16 bora kwani itakuwa na maana kuwa taifa la Benin na taifa la Angola hayajafikisha alama 3 kama za Harambee stars na hivo basi Kenya itafuzu kama nafasi ya tatu.

Kwa sasa, mataifa ya Senegali, Misri, Algeria,Uganda,Cameroon, Mali, Morocco, Ivory Coast, Madagascar na Nigeria. Mechi za raudi ya 16 zitanza tarehe 5 julai.