PATANISHO: Mama mkwe alificha mke wangu na watoto

Nickson Odongo alituma ombi apatanishwe na mama mkwe ambaye alichukua mke wake na watoto na kuwaficha na kila akimpigia simu hashiki.
"Ilikuwa mwaka jana krismasi ambapo mke wangu aliniomba ruhusa aende kumsaidia mama yake kwa sababu alikuwa na wageni

Baada ya muda alikaa na nikamtumia nauli lakini hakurudi, nilipompigia simu sikumpata, nilipompigia mama mkwe simu hakushika simu yangu.

Ninapoongea na baba mkwe yeye huniahidi kwamba atasuluhisha mambo hayo.  Sijawahi kuambiwa aliko mwanangu aliyekuwa na miezi  sita.

Nilikuwa nataka kujua vile wanaendelea, kwa sababu hata jana nilipiga simu ya baba mkwe lakini hakushika. Nilikuwa nimepanga kwenda kulipa mahari mwezi wa nane lakini hayo yametokea" Bwana Odongo Alizungumza.

Mama mkwe wake alipopigiwa simu aliongea na kisha kukata baada ya muda alizima na hakupatikana tena.

Je ushauri wako kwa bwana Odongo ni upi?