PATANISHO: Niliachana na mume wangu baada ya kumpoteza mtoto wangu

Rosemary,22, alituma ujumbe apatanishwe na mume wake Dennis,30, ambaye walikosana mwaka jana baada ya kumpoteza mtoto wake, na mume wake kumtishia kumdunga kisu aendapo angempata  kwa nyumba.
"Ilikuwa mapema mwaka huu nilimpoteza mtoto wangu na kuenda kumzika nyumbani kwa mzee wangu baada ya mazishi  mume wangu alibadilika

Waliongea kwa lugha yao kwa maana, mimi si wa kabila lao, tuliporudi Nairobi alianza kulala na nguo hata nikimuonyesha mapenzi hakuwa anakubali

Nikimshika alikuwa ananiambia nisimshike, mimi si bibi yake na sifahi kumshika kwa maana mimi si mke wake, siku moja alinishikia kisu na kunishauri asinipate nyumbani mwake kesho yake akitoka kazi

Nilimuuliza ni nini mbaya na kuniambia kuwa ana mke na mimi si mke wake." Alieleza Rosemary.

Dennis alipopigiwa simu alikataa kushika na hata kukata,

Yote tisa kumi Rosemary alikuwa na haya ya kumwambia mumewe.

"Kama umeoa nakuombea Mola umpe mwanamke huyo heshima na husije kumfanyia vile ulinifanyia, na kwa maana mtoto wangu yuko kwenu siku moja utakuja kunitafuta

Nami nilikupenda kwa roho yangu yote." Alisema.

Rosemary alisema kuwa mumewe hapendi kushauriwa ukweli na mtu yeyote, kwa uhndo zaidi tembelea mtandao wetu wa kijamii wa youtube.