gidi

PATANISHO:Mke wangu aliniacha kwasababu ya ulevi

Katika kitengo cha patanisho leo Duke,36, alituma ujumbe apatanishwe na mke wake ambaye walitengana miaka mitatu sasa, wamebarikiwa na watoto watatu na mkewe akaenda nao kwao.

Bwana Duke alikuwa na haya ya kusema kuhusu kutengana kwao,

PATANISHO: Niliachana na mume wangu baada ya kumpoteza mtoto wangu

“Tulitengana na mke wangu kwa ajili niliwa nalewa sana, hata nikumuoa nilikuwa nanywa sana, kuna wakati nilienda kutafuta kazi niliporudi nyumbani nilipata amehama mahali tulikuwa tunaishi na kwenda

Wakati huo nilikuwa na shughulikia familia, nilipompigia simu aliniambia nimpe muda apumzike, si mara moja bali mara nyingi sana nikimpigia huwa ananiambia tu hivyo.

Nilipopigia wazazi wake walikuwa upande wake lakini ndugu yake hana shida yoyote.” Duke Alieleza.

Alizidi kueleza,

“Kuna wakati ambao nilikuwa nampigia simu anakosa kushika, wakati huo huo nililewa chakari nikampigia simu na kumuongelesha vibaya.

Nilidhani kuwa alipata mipango ya kando, kila ninapoenda mahali anafanya kazi uwa anakimbia kila mara, wakati mwingine huwa ananipigia simu ili nitume pesa za watoto.” Alisimulia.

Mkewe alipopigiwa simu hakushika. Je maoni yako kwa bwana Juma ni yapi?

 

Photo Credits: radiojambo

Read More:

Comments

comments