Patanisho: Mke wangu alitoroka nyumbani na amekataa kurejea

Baba Daniela, 37, ameomba apatanishwe na mkewe mama Daniela ,31, ambaye aliondoka nyumbani kwake mwezi februari kama hawajakosana kwa vyovyote vile kulingana naye Baba Daniella.

"Tumekuwa na uhusiano na mke wangu na tuko na mtoto mmoja.Jioni moja nilitoka kazini na nilipofika nyumbani sikumpata wala mtoto.

Mimi nilidhani amenda matembezi na nilipomuuliza alinieleza kuwa atarejea na mimi sikusita kumgonjea. Hata hivyo,tangu wakati huo mwezi februali hajawahi rudi na nilipompigia simu amaekuwa akisema atarudi mwezi wa nane. Mwezi wa saba alifunga simu jambo linalo nikosesha amani."

Mama Daniela kwa upande mwingine amekanusha madai yake baba Daniella kwa kusema kuwa hakutoka nyumbani kwake bure.

 "Gidi acha nikwambie, mimi sikutoka kwake bure. Matusi aliyokuwa akinipa yalinikosha mimi na nikaamua kwenda zangu. Amekuwa akileta wanawake wanalala kwa kitanda naye na mimi nalala nje. Wakati mwingine hataki kulala kwa nyumba. Mimi  nimechoka na nimeamua kuishi kivyangu.Nilijipanga kwa muda mrefu kutoka kwake na wakati kamili ulipofika mwezi februali mimi nilijiendea zangu na kumwacha kwake."

Mama Daniela amesema kuwa mumewe alikuwa na kiburi kwani hakuwa anataka kumsilikilza hata wakati mmoja.

"Kila wakati anaonakanga akiwa sawa,haonangi makosa yake. Kilicho nifanya nisimwambie sitarudi ni vitisho vyake vya kujiua."

 Mama Daniela alikataa kurudiana na mumewe na kusema kuwa yeye tayari ashaendeleza maisha yake na hivyo mumewe anapaswa kumshau. Hata hivyo, baba Daniela amemwambia mkewe kuwa yeye yuko tayari wakati wowote.

"Mimi na wewe ndio pekee tunaelewa umuhimu wa ndoa hii. Hivyo ningeomba tu turudiane na tuinishi vizuri na amani kwa sababu nakupenda sana. Sitao tena na nataka ujue kuwa nakungoja kwa sababu naamini kuwa utarudi kwangu siku moja."

"Hayo maneno ungeyatumia ukiwa na wakati. Kwa sasa nisahau na uendelee na maisha yako. Nimeamua kuishi bila mwanaume maishani mwangu," Mama Daniela alisema.