PATANISHO:Niliachana na mke wangu kwa sababu alichapwa na mamangu na dadazangu

Ken,24, kutoka Tongaren alituma ujumbe ili apatanishwe na mke wake cylvia,21 waliooana kwa mwaka mmoja na kisha kuenda kwao kwa sababu ya kucharazwa na mama yake.
"Mke wangu tuliachana kwa sababu alichapwa na mama yangu na dada zangu, niipoenda kuwauliza ata mimi walinichapa baada ya hapo walienda kumkimbiza na mawe kwa sababu nilienda kuwauliza kwanini walifanya kitendo hicho

Walikuwa wanamchapa nikienda kazini, walisema kuwa mke wangu aliwasengenya ndio maana walimchapa kichapo cha mbwa." Alieleza Ken.

Ken alikiri kuwa baada anampenda mkewe sana kama maharagwe.

Mkewe alipopigiwa simu alikuwa na haya ya kusema,

"Kwanza mwenye alinichapa sana ni dada yake ambaye alikuwa ameolewa na akarudi kwao, walinichapa huku wakidai kuwa nimewasengenya lakini sijawahi wasengenya

Mke wake w kwanza walimchapa tu hivyo akaenda kwa ni kama hawataki kijana wao aoe, mtoto wangu wa kwanza nilimzaa na operesheni

Walinichapa mpaka damu ikaanza kutiririka mahali ambapo nilikuwa nmefanyiwa operesheni kwa sababu sikuwa nimepona sana." Alieleza Cylvia.

Aliongeza na kusema,

"Waliponiumiza mama yangu mzazialiniambia nirudi nyumbani ili niweze kupona, kama Ken anataka nirudi atoke kwa wazazi wake na kuishi kwingine nitarudi kwa maana bado namtambua kama mume wangu." Alinena.