PATANISHO: Mume wangu amekuwa akibadilisha wanawake kama nguo

Katika kitengo cha patanasho mwanamke Sharon,22, alituma ujumbe ili apatanishwe na mume wake Andrew,24, baada ya kukosana miezi mitatu iliyopita kwa sababu mume wake anapenda mpango wa kando.

Wawili hao wamekaa katika kwa mwaka mmoja na kubarikiwa na mtoto mmoja.

"Nilikosana na mume wangu kwa sababu alikuwa na mipango ya kando, mara nyingi alikuwa anakuja nyumbani akiwa amelewa na kuanza kuongea na wanawake 

Nilipomuuliza aliniambia nikitaka nirudi kwetu, siku moja aliniambia niende nikasalimie mama yangu niliporudi nilipata ameoa mwanamke mwingine

Kuumuliza tena aliniambia nikitaka kukaa nikae nilikaa na mke mwenza wangu lakini ilifika muda akaenda

Baada  muda mfupi niligundua ako na mwanamke mwingine nikachukua nambari yake ya simu nikampigia na kikamualika kwa nyumba." Alisimulia Sharon.

Bwana Andrew alipopigiwa simu alisema yuko kazini na hana nafasi ya kuzungumza, Sharon alimsihi mumewe atakama anponda raha ajue na aweke kwa akili kuwa mtoto wake anamhitaji.

"Najua anasikiza radiojambo nataka kumwambia kuwa mtoto wake anamhitaji ata akila raha aje ajue hivyo." Alisema Sharon.

Ni mtindo na tabia ambayo imeenea sana katika kizazi cha sasa, vijana wengi wanaingia katika ndoa bila hata ya kuwa tayari.

Na baada ya muda wasumbuana na kuachana jambo ambalo linafanya watu wengi kujiua, je ushauri wako ni upi kwa mtindo huu?