PATANISHO: 'Akileta ujinga nitatoroka tena', asema Bi Pauline baada ya kumsamehe bwanake Lawrence

Lengo la patanisho katika stehseni ya Radio Jambo ni kuleta pamoja wapendwa wawili walio kosana. Na hivi leo, Monday Februrary 20, Lawrence aliye kosea mke wake aliomba wapanishwe.

Lawrence, anaye miaka 24, amekaa na mke wake Pauline kwa miaka mnne, na akapachika mwana dada mwingine mimba, huku Bi Pauline akitorokanyumba ya bwanake.

Licha ya kukosana Lawrence hadi sasa hajawahi patana na bibi yake aliyetoroka. Wametengana kwa miaka mmoja.

Lawrence anahisi mpango wa kando ndiye aliharibu ndoa yake.

'Nini ilitokea' Gidi aliuliza Pauline kupitia simu.

Pauline: 'makosa kinyumbani ndio ilifanya tukosaane. Alikuwa na wasichana wengi, na mimi nilishindwa ni nini anachotaka. Nishanga kwa sababu niliambiwa ni wengi, na wengine wananitusi kwa simu'.

Gidi: sasa hao ni baby mama?

Pauline: mimi sijui. Aliniwacha na mtot na hakuwa anajibika na kushugulika. Hakuwa anapenda mtoto wetu pia, na sikuelewa.

Gidi; Kwani alikuwa anashuku si wake?

Pauline; mimi sijui. Kile imebaki ni kupanga safari uombe msamaha ya wazazi wake. Akileta ujinga nitatoroka tena, awachane na madrama.

Skiza kanda ifuatayo, upate uhondo;