Patanisho: Alikasirika na kumtumia mkewe wangu jumbe zetu zote

Bwana Nicolas 28 aliomba apatanishwe na mkewe bi.Evelyn 26 baada ya mkewe kuamua kufunga virago vyake na kurejea kwao mjini Meru na kumwacha Nicolas Mjini Mombasa.
"Nilikuwa na nazungumza na mwanamke mwingine kwenye mtandao wa Facebook. Nilimwalika mjini Mombasa aje tupatane lakini alipofika mie sikwenda kumwona. Mwanamke huyo alikasirika na kutumtumia mkewe wangu jumbe zetu zote."

Bwana Nicolas amesema kuwa hakuwahi fanya jambo lolote na mwanamke huyu mwingine anayetoka maeneo ya Nyeri.

Bi. Evelyn kwa upande mwingine anasema kuwa bwana Nicolas alikuwa amemkosea mara tatu huku akimsamehea mara zote tatu hizo.

"Mimi sitarudi kwako mpaka unikujie.Kama unanipenda funga unikujie."

Kulingana naye Evelyn, bwana Nicolas alikuwa amezoea kudanganya licha ya kuwa yeye alikuwa mwaminifu.

"Akibadilisha tabia basi mimi bado nampenda na ntamrudia ila kwanza lazima akuje nyumbani azungumze na wazazi wangu ili anihakikishie kuwa hatarudia hizo tabia zake," alimaliza Evelyn.

Nicolas alikubali kumwendea mkewe Mjini Meru siku ya Ijumaa.