patanisho.fresh

PATANISHO: Alinichapa na kuniumiza mbavu na kichwa

Paul mwenye miaka 32 aliomba kupatanishwa na Martha mwenye miaka 28. Wawili hawa wamekua kwenye ndoa kwa miaka tisa lakini Paul akamchapa na kumuumiza Martha, ambaye aliondoka.

PAul alieleza kwamba;

“Mke wangu alienda, nilikua nimemfungulia kazi ya kuuza viazi. Nilikua nimetoka mazishi nikapata amekasirika akidhani nimetoka kwa wanawake, akaenda sokoni akaniachia mtoto, nikachukua mtoto nikapelekea mwanamke mwingine ambaye ni Cousin yangu.

Nikiwa nakunywa pombe, bibi akaniambia mtoto hajakula. Nikiongea na mwanamme mwingine, akadhani nilikua namuongelea, akanitusi, nikamtandika makofi. Nilikua nimekasirika na kulewa. Mimi ndio nilikua na makosa.Martha naomba unisamehe.”

PATANISHO: Nime move on na maisha na haturudiani!

Martha alimjibu Paul;

“Alinipiga na kunifanya madharao, akanikanyaga, mbavu na kichwa akaniumiza kabisa hata sasa hivi sijapona.Pole yako mimi sitaki ulinishapa na haukuwahinisaidia hata hospitali. Sitaki nimekataa. Nitakupatia miaka tano ujirekebishe.Nimechoka na kulia na kuchapwa kila siku.Mimi nishatosheka kuolewa”

Sikiza mawasiliano yote kati ya Paul na Martha kwenye link ifuatayo;

Photo Credits: File

Read More:

Comments

comments