PATANISHO: Alisema ataniendea kwa mganga ili niwe wake - Mercy

Bwana Mungai alituma ujumbe akiomba apatanishwe mpenzi wake waliyekosana miaka miwili iliyopita.
"Mamake hakuwa anataka mimi naye tufunge ndoa na hata tukichumbiana naye mamake hakuwa anataka. Tulianza uhusiano mwaka wa 2017 na ikafika mahali nikamchukua tukaanza kuishi pamoja kwa wiki moja.

Hapo mamake alinitumania watu wakaniumiza na kunifikisha kwa chifu kuhusu msichana wake na hata sasa hivi huwa hatuzungumzi." Alieleza Mungai.

Aliongeza akidai wakichumbiana na Mercy, alikuwa na miaka 23 naye akiwa na miaka 25. Hilo ni kinyume na kile Mercy alisema kwani alidai walipopatana alikuwa na miaka 17 na sasa hivi ana 22.

Wawili hao hawazungumzi kwa sasa kwani kila anapompigia simu hajishiki simu wala hajibu jumbe zake. Licha ya hayo, Mungai angetaka kuzungumza na mpenziwe ili ajue kama bado anampenda.

"Na wewe si una bibi kwanza? mbona unanifuatilia?" Mercy alimfokea Mungai pindi tu aliposkia sauti yake.

Aliongeza,

Mungai ana bibi ambaye alijifungua mtoto na kumuita Mercy mimi sitaki kuwasiliana naye kwani nitaharibia bibi yake ndoa."

Mercy kwa upande wake alisema hajaolewa bado ila hawezi rudiana na aliyekuwa mpenzi wake.