PATANISHO : Alitaka kulipa gunia ya mahindi kama mahari, Wilkister asimulia Gidi

Screenshot_from_2019_12_13_02_16_21__1576222395_32144
Screenshot_from_2019_12_13_02_16_21__1576222395_32144
Bwana Dancan Mbasu, 31, amesimulia kisa cha kuachwa na bibi pamoja na watoto wawili baada ya kuonyesha vitendo vya kutoka kimapenzi na wanawake wengine.

Mbasu alipiga simu katika kipindi kinachoruka kila asubuhi cha Patanisho ili apate kusaidika katika juhudi za kuileta pamoja familia yake.

https://www.instagram.com/p/B5_9WDegMl6/

Katika simu ya dakika 7 na ushei, Dancan amesimulia masaibu yake na mke wake Wilkister.

"Shida ilianzia kutoka 2017 wakati tulianza kuishi pamoja. Kilichosababisha kutoelewana ni kitendo changu cha kuenda nje ya ndoa nikapata mtoto..." Amesema Mbasu.

Dancan amesema kuwa sababu ya kuchepuka ilichochewa na kuwa alifanya kazi mbali na mkewe.

"Alikuwa mbali na mimi. Alitoroka mwaka huu ukianza. Tumekuwa tukiongea na mara ananihaidi kuwa atarudi. Kidogo akakuja mwezi wa sita na akanifunia na msichana ndani ya chumba na hapo akaenda tena..." Mbasu alisimulia Gidi.

Alipopigiwa simu na Gidi, mkewe Wilkister, 28 amefunguka A-Z masaibu aliyoyapata katika ndoa na bwana Mbasu.

"Wacha nikuambie Dan kitu cha kwanza ulinichukulia kimadharau. Tulikuwa tunang'ang'ana na maisha. Vile ulipata pesa ukamea pembe. Tulitoka chini hata hatukuwa na kitanda ama mattress..." Amesema mkewe.

https://www.instagram.com/p/B5w0yVwFBk8/

"Yaani ulichukulia kwetu ni maskini. Mpaka hiyo kitu huwa inanisononesha sana. Unakumbuka ukiambia mamangu unaweza ukaninunua na gunia ya mahindi? Inafika mahali mpaka nashangaa sana. Mpaka wazazi wangu wakasema kuwa huyo mwanamume hafai kuwa mume wangu..." Amejuta Wilkister.

Wilkister amemtaka mumewe afike nyumbani kwao na kuomba msamaha kwa wazazi wake ili wapate kumsamehe.

Aidha, mwanadada huyu amesema kuwa atarudi iwapo mumewe atafanya hivyo na kubadilisha mienendo yake.