ghostmuleeandgidi

Patanisho: Alitoka na ugali nilipoenda kumtembelea

Bwana Dennis Gisaka, 35 aliomba apatanishwe na mkewe Jackie 31, baada ya mkewe kutoroka ndoa yao iliyokuwa imedumu kwa zaidi ya miaka kumi.

“Mkewe wangu alikosana na wazazi wangu mwaka wa 2015 mwezi disemba na  kisha tukaenda na kusuluhisha hayo mambo. Siku nne baadaye alitorokea kwao na nilipomwendea yeye alisema hatarudi tena.”

Bwana Dennis anasema kuwa mkewe alitoroka na watoto wao wote ila yeye alimwendea mwanae wa kiume kwani mila na destruri hazikubali mtoto wa kiume kuishi na nyanyake. Hata hivyo, mwaka mmoja baadaye Dennis alimpata tena mkewe.

“Nilimtafta na siku moja nikampata Kitengela. Alinikaribisha na kunipikia ila niliposema ntalala kwake alikataa na akatoka na ugali  nami nikasema sitoki huko. Yeye alienda kulala kwa jirani yake na mimi nikalala kwa kitanda chake. Niliamka asubuhi na kuchukua tuktuk na nikambebea vitu zake zote.”

Jackie, mkewe Dennis hata hivyo ameapa kutomrudia bwanake,

“Huyo jamaa alinikosea sana. Alikuja kwangu akabeba kila kitu. Mimi ni kama ile wimbo ya dunia haina huruma na mimi sina huruma yoyote kwako. Huyu jamaa siku moja aliambia babangu akuje anioe na sasa wazazi wangu wameniambia nikimrudia mimi sio mtoto wao tena.”

Jackie anasema kuwa Dennis hawezi sameheka na hivyo yeye anachokifanya sasa ni kuwataftia wanawe karo na hataki tena mambo yake.

Soma mengi hapa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments